Jumanne , 12th Nov , 2019

Uongozi wa Hotel ambayo ilitokea vurugu ya msanii Ebitoke, baada ya kuvamia mkutano wa msanii mwenzake Yusuph Mlela, amezikanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikieleza kuwa uongozi huo ulikuwa unajua kama baadae kutatokea vurugu katika mkutano huo.

Akizungumza leo Novemba 12, 2019, Meneja wa Hoteli ya Protea, Suleiman Victor, amesema kuwa hawakuwa na taarifa zozote zinazohusu ugomvi huo na kwakuwa wamekwishalipwa fidia ya meza yao iliyoharibika, hivyo hawatochukua hatua za kisheria kwakuwa hakuna athari yoyote iliyojitokeza kwa mgeni aliyekuwa akitoka ama kuingia.

"Sisi hatukuwa na taarifa kwamba anaweza kufanya drama, hata kama angetuambia hivo sisi tusingeweza kuruhusu na kitu ambacho tunaweza kushukuru, wakati hizo vurugu zinatokea hakukuwa na mgeni anayetoka ama kuingia" amesema Meneja.

Kwa mujibu wa Meneja huyo, jana jioni siku ya Novemba 12, 2019, baada ya ugomvi kutokea, msanii Yusuph Mlela,  amelipa kiasi cha dolla 500 za Marekani, kama fidia ya meza moja iliyoharibika.