Jumatatu , 19th Mar , 2018

Rais wa Manzese, Madee amesema hana mpango wowote kwa sasa wa kuachana na muziki kama watu wanavyofikilia katika vichwa vyao, kwa madai muziki ndio maisha yake hivyo atafanya mpaka pale kifo kitakapokuja kumchukua.

Madee ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha 'FRIDAY NIGHT LIVE' (FNL) inayorushwa na EATV baada ya msanii huyo kuonekana kusajili wasanii wake wapya kila kukicha jambo ambalo lilipelekea baadhi ya watu kudhania pengine Madee ana mpango wa kuacha na kuimba kwa sasa.

"Music my life yaani toka napata akili naanza muziki nikasema nitakuachana na kazi hii labda siku ambayo nitakuwa nimemaliza pumzi zangu 'kufa'. So hata kama ntakuwa sipeleki nyimbo kwenye stesheni mbalimbali, si-rekodi lakini ntakuwa bado ntakuwepo nimeegemea kwenye biashara ambayo itakuwa inahusiana na muziki", amesema Madee.

Mtazame hapa chini Madee akiendelea kufunguka mengine zaidi.