Solomon Mkubwa azungumzia afya ya Rose Muhando

Jumatatu , 15th Apr , 2019

Muimbaji  maarufu wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando, jana jioni ameagwa katika hospitali aliyokuwa amelazwa nchini Kenya baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Solomon Mkubwa akiwa na Rose Muhando.

Kupitia video iliyochapishwa na Solomon Mkubwa, inamuonesha Rose akiimba na kumshukuru Mungu kwa kumponya akiwa na waimbaji wenzake wa nyimbo za injili, Betty Bayo pamoja na Solomon Mkubwa.

Solomon amepost picha akiwa na Rose na waimbaji wengine na kuandika, “Mungu mkubwa, Rose Muhando amekua vizuri. Malkia Rose yuko poa sasa”, ameandika Mkubwa.

Rose Muhando aliibua hisia kali miongoni mwa mashabiki wake nchini Kenya na Tanzania miezi minne iliyopita alipoonekana jijini Nairobi akiwa na majeraha makubwa huku akiombewa na mhubiri jijini humo, James Nganga.

Katika picha hizo, majeraha aliyokuwa nayo hayaonekani tena na anaonekana ni mchangamfu kabisa na hali yake ya kiafya ikionekana kuimarika.