Stamina afunguka walioiba hela za rambirambi

Ijumaa , 22nd Feb , 2019

Msanii wa hip hop bongo Stamina, amefunguka juu ya watu walioiba pesa za rambirambi za msiba wa Godzilla na kusema kuwa kitendo hicho ni laana huku akiwataja kuwa watakuwa ni wasanii wenzao.

Akizungumza na Big Chawa kwneye Planet Bongo ya East Africa Radio, Stamina amesema kwamba haiwezekani mtu ambaye si msanii akawa ndiye aliyeiba pesa hizo, kwani waliokuwa kwenye kamati na waliokuwa wakishughulikia suala la rambi rambi ni wenyewe wasanii.

"Kupiga hela ya Godzilla ni sawa na laana ambayo sidhani kama itafutika, kwa sababu Zizi alikuwa mwana, ifike time tafuta hela yako babu, mpaka mtu afe ndio utafute hela? Halafu hizi stori wanatuchoresha, kwa sababu 'by any means' walioshiriki ni wasanii, kwa hiyo waliopiga watakuwa ni wasanii, hawezi kuwa eti Juma Abduly wa mtaani huko ndio kapiga, no! Kwenye ile ile kamati aliyepiga ni msanii”, amesema Stamina.

Pia Stamina amewageukia watu walio hack acount ya Godzilla ya Instagrama na kusema kwamba kufanya hivyo sio kitu cha kiungwana na ujinga, kwani acount hiyo ingekuwa kumbukumbu kubwa kwa wenzake na hata kwa mtoto wake aliyemuacha.

Huo ni ujinga ambao nimeuona, sio kizazi babu, akaunti ya marehemu unachukuaje! Kwani ukiiacha inakuwa nini, si unaiacha tu. Watu hawajui, zile caption ndio kumbukumbu zake, unataka tumkumbuke kwa nini?Yyule mtoto wake unataka tumuoneshe vitu gani, yule anatakiwa aje ajue baba yake alikuwa mtu wa namna gani, akiangalia zile post, ila dah!! Wabongo bwana, wabongo bado sana”, amesema Stamina.

Ikumbukwe kuwa mwezi huu tasnia ya bongo fleva imepata pigo kwa kufiwa na rapper Godzilla, baada ya kuumwa kwa muda mfupi.