TAMASHA LA KIBOKO YAO KUTIKISA DAR

Jumanne , 13th Jan , 2015

Kampuni ya simu ya mkononi ya tiGO imetangaza kuandaa tamasha kubwa kabisa la muziki la aina yake lijulikanalo kama “Kiboko Yao” litakalofanyika Januari 24, mwaka huu Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni.

Christian Bella (Katikati) moja ya wasanii watakaotumbuiza katika onyesho la Tigo Kiboko Yao Music Concert tarehe 24 mwezi huu pale Leaders Club akiwahakikishia mashabiki wake uwepo wake katika tamasha hili kubwa leo.

Akiongea leo katika mkutano wake na waandishi wa habari Meneja wa Chapa wa tiGO William Mpinga, amesema tamasha hilo litatumbuizwa na wasanii 18 wakali, linaenda sambamba na kutambulisha huduma mpya ya tiGO Music itakayowaletea wateja wao burudani ya muziki kupitia simu zao.

Katika Mkutano huo na waandishi wa habari pia walikuwemo baadhi ya wasanii watakaopanda jukwaani katika tamasha la Kiboko Yao, akiwemo Diamond Platnumz, Ali Kiba, Christian Bella, Ben Pol, Mwana FA, Fid Q, Isha Mashauzi, Vanessa Mdee, Yamoto Band pamoja na bendi kongwe za Msondo na Sikinde.

Kwa taarifa zaidi endelea kutazama EATV na kusikiliza East Africa Radio kila wakati, tiGO Music Concert Kiboko Yao Januari 24 pale Leaders Club. historia mpya ya burudani ya viwango kuandikwa nchini.