Tamko la Alikiba kutikisa tasnia ya muziki leo

Ijumaa , 8th Nov , 2019

King Of Bongo Fleva Ali Kiba ametangaza kutoa tamko rasmi mbele ya wanahabari, leo Novemba 8, 2019 litakalofanyika RAMADA ENCORE, Posta Jijini Dar Es Salaam.

Eneo ambalo Alikiba atatolea tamko leo.

Tangazo hilo la tamko rasmi litakuwa 'LIVE' kupitia kipindi cha eNewz ya East Africa Television, kuanzia saa 12:00 jioni, East Africa Radio na kupitia mitandao ya kijamii kwenye ukurasa wa Facebook  na YouTube (East Africa TV).

Baada ya tangazo la tamko hilo kutakuwa na hafla 'party' iliyopewa jina la "Unforgettable After Party" katika moja ya ukumbi wa starehe 'Elements' uliopo Masaki Dar Es Salaam.