Jumapili , 27th Oct , 2019

Msanii mkongwe wa Bongofleva TID ameweka wazi kuwa kwasasa ametulia na ameacha mambo ya ugomvi kwasababu amezuiliwa kufanya hivyo na msanii anayemheshimu sana.

TID akiwa na Lady Jay Dee

TID amefunguka hilo kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, ambapo amemtaja msanii Lady Jay Dee kuwa ndiye mtu aliyemzuia kugombana na watu kama ilivyokuwa zamani.

'Dada yangu Lady Jay Dee amenizuia sana kugombana na watu kwahiyo sasa hivi nimekuwa mpole sana sio kama zamani ilivyokuwa jino kwa jino', alisema TID.

Mkali huyo pia ameweka wazi kuwa Chemistry yake na Jide kwenye muziki ndio bora zaidi kuwahi kutokea na ndio maana hata ngoma yao mpya 'Any More' inafanya vizuri na ipo kwenye namba 10 Trending katika mtandao wa YouTube.