Ijumaa , 22nd Feb , 2019

Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Khaled Mohamed, Maarufu kama TID amekataa kuitwa jina la 'Mnyama' ambalo alianza kutumia miaka kadhaa iliyopita.

TID ambaye anajulikana kwa majina mengi yakiwepo, Kigogo, Warioba, Mnyama na mengineyo amesema chanzo cha kulikataa jina lake hilo ni kutokana na  kwamba watu wengi wameanza kulitumia.

"Naitwa TID kuanzia leo sitaki kuitwa mnyama kila mtu nae kawa mnyama sasa hivi, sina unyama wowote 'I am a changed Person'. Niiteni 'Top' tu kama zamani 'pliz' tusije gombana mimi sio mnyama, niko binadamu tu", ameandika TID katika ukurasa wa Instagram.

Machi 2017, TID alilikataa rasmi jina la TID, ambalo ndilo lililompatia umaarufu na kupendekeza aitwe jina lake alilopatiwa na wazazi wake au 'Mnyama' kwa madai kwamba wanaopaswa kumuita jina hilo ni watu wa mikoani tu.

"Sitaki watu waniite TID, niite Mnyama nikiwa mtaani mimi ni Khalid, jukwaani ndiyo TID. Tatizo jina la Top in Dar limekuwa 'too casual' sana mpaka nachukia. tuwaachie watu wa mikoani huko ndiyo waniite TID lakini wa hapa mjini we ukinisalimia niite tu Khalid inatosha", alisema TID.