Tommy Flavour afunguka siri ya kumtuliza Lyyn

Jumatano , 16th Sep , 2020

Msanii wa BongoFleva kutokea lebo ya Kings Music Records Tommy Flavour amefunguka kuwa kilichosababisha kumtuliza Official Lyyn kwenye mahusiano yao ni misingi ya ukweli na utofauti.

Tommy Flavour na Official Lyyn

Akizungumzia kuhusu mwanzo wa mahusiano yao kwenye kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Tommy Flavour amesema penzi lao lilianzia studio baada ya kukutana kisha wakawa marafiki waliopitiliza.

"Kitu ambacho nimefanya hadi kuweza kutulia na Official Lyyn ni misingi ya kuwa 'real', kingine labda kuna vitu tofauti ameviona kutoka kwangu ndiyo maana nimetulia naye, nakumbuka tulikutana studio na tukaanza urafiki ila urafiki wetu ukazidi, mahusiano yetu yana muda wa miezi 7 tangu tuwe pamoja" amesema Tommy Flavour