Ijumaa , 14th Oct , 2022

Mrembo Tuerny amejitosa rasmi kwenye mziki akieleza kuwa lengo lake ni kuufikisha mziki mbali zaidi.

Picha ya mrembo Tuerny

Tuerny ameshea ujumbe huu kuhusu kuingia kwake kwenye mziki.

"Safari yangu ya mziki inaanza leo ramsi Oct 14, Hii ni historia kwangu ni siku ambayo niliyokuwa naisubiri kwa hamu sana ifike, Naomba mnipokee kwa mikono miwili sitowaangusha".

"Nimekuja kuongeza nguvu kwa upande wa wasanii wa kike na kwa game yote kiujumla. Lengo ni kuufikisha mziki wetu mbali zaidi".