Jumamosi , 27th Apr , 2019

Video Vixen marufu bongo, Tunda 'the Boss babe', ameweka wazi hisia zake juu ya mchekeshaji Piere, akisema kwamba mchekeshaji huyo ndiyo kitulizo chake kwa sasa.

Akifunguka hayo, Tunda amesema kwamba Piere ndiye mtu pekee kwa sasa anayeweza kumtoa msongo wa mawazo (stress), na kwamba iwapo yuko mbali naye, basi yuko tayari amfungie safari kumfuata aliko ili afurahi naye.

Alichokisema Tunda 

 

“Unajua unaweza ukawa na mawazo na hujui yatatoka vipi, kwa kweli kwa mimi Pierre anamaliza mawazo yangu yote. Nikiona sipo sawa, huwa naona bora nimfuate popote alipo ili tu niwe sawa,” amesema Tunda.

Wawili hao hivi karibuni walionekana kuwa karibu zaidi, na kuanza kuibua maswali kwa wadau kuwa huenda kuna jambo linaendelea kati yao ambalo si la kawaida.