Jumatatu , 28th Oct , 2019

EATV & EA Radio imepiga stori na staa wa BongoFleva Nedy Music, ambapo amefunguka kuhusu 'Lifestyle' yake kwenye upande wa mavazi, muonekano binafsi na wasanii kupenda kuvaa hereni masikioni.

Akizungumzia issue ya kuvaa hereni au vipuli  kwa wasanii hali ya kuwa yeye ni muislam Nedy Music amesema, sasa hivi ukiangalia dini utakosea vitu vingi vilivyopo duniani.

"Mimi kila kitu nachohisi kinafaa kwangu naweza kukivaa au kukiweka, kwa sababu ukiangalia dini sasa hivi utakuwa unakosea kwa vitu vingi vilivyopo duniani, kwahiyo yote kwa yote ni kuweka sawa tu kama leo navaa cheni kesho sitavaa, ila kawaida kwa msanii au mtu  yeyote anayetaka kupendeza" ameeleza Nedy Music.

Pia Nedy Music amezungumzia suala la kuhusishwa kuchukua nafasi ya  Juma Jux na G-nako Warawara, kwenye upande wa kuvaa kwa sababu wawili  hao wanaaminika kama ndiyo wasanii wanaongoza kwa kuvaa Bongo.

"Mimi sivai kwa ajiili ya kuchukua nafasi ya mtu yeyote yule, bali navaa Nedy kama Nedy nikiamini kwamba, nataka kuvaa vile nakuonekana vizuri kwa watu ambao wanani-support na wanaoniangalia pia".