Ijumaa , 3rd Jul , 2020

Kupitia kipande cha video fupi aliyo-post msanii Marioo "Toto Bad" ameeleza kuwa ukimtoa Whozu staa mwingine ambaye anafuatia kwa kuumizwa na kuonewa kwenye mapenzi ni Lulu Diva.

Msanii Marioo upande wa kulia, kushoto ni Lulu Diva

Marioo amefahamisha hivyo baada ya kupata bahati ya kuonana na Lulu Diva ambaye amemuuliza kwanini  ameandika wimbo ambao baadhi ya vitu vinamuhusu yeye.

"Aaaaam Lulu Diva ni moja kati ya mastaa ambao washawahi kuumizwa au kuonewa katika mapenzi tukiachana na Whozu, sasa leo tulipata bahati ya kuonana akawa ananiuliza nimewaza nini mpaka nikaandika huu wimbo maana ndiyo wimbo anauskiliza kutwa nzima kwa hiyo nikawa namuelezea baadhi ya vitu kuhusu wimbo" ameeleza 

Kwa sasa Whozu yupo kwenye mahusiano na video vixen Tunda, na Lulu Diva bado hajaweka mahusiano yake wazi japo awali aliwahi kuhusishwa kuwa na TID, Rich Mavoko na Jaguar.