Alhamisi , 9th Jul , 2020

Gumzo za taarifa za kupigwa kwa Shilole kutoka kwa mume wake Uchebe zimekuwa nyingi kuanzia kwenye vyombo vya habari, haki za binadamu "HRC", mitandaoni, mastaa, wafanyabiashara na baadhi ya viongozi wa kisiasa.

Msanii Shilole upande wa kulia, kushoto ni Uchebe

Kupitia EATV & EA Radio Digital tunaangalia upande wa kisheria kuhusiana na tukio hili la ukatili kwenye ndoa au mahusiano yoyote, na Wakili Jebra Kambole amefananua kwa kusema hukumu ya kesi kama hii huenda ikawa ni kifungo cha miaka mitano jela.

"Katika mtazamo wa kisheria kuna mambo manne yanayojitokeza kwanza ni kukiukwa kwa haki za msingi za binaadam kwa sababu kila mtu ana haki ya kuwa huru, kuishi na kutopigwa kwa namna hiyo, pili mke na mume wanaweza kutendeana makosa ya jinai na sheria imetoa muongozo kwenye eneo hilo

"Ni kosa la jinai kumdhuru au kumjeruhi mtu hata kama ni mkeo, mumeo au mtoto, sheria ya makosa ya Jinai sura ya namba 16, kifungu namba 240 na 241 kinajinaisha kosa la namna hiyo na ikitokea limetendeka mahakama inaweza ikatoa adhabu ya miaka mitano kama endapo kosa hilo limetoa madhara kwenye mwili wa mtu" ameongea Wakili Jebra Kambole 

Zaidi tazama akieleza kwa kina zaidi hapa chini kwenye video.