Msanii wa BongoFleva Matonya
Sasa kwa upande wa msanii wa BongoFleva Matonya amefunguka kusema sababu ya yeye kutopenda kuonekana kwa watu ni uvivu, pia amekiri uvivu umemsaidia sana kwenye maisha yake hadi alipofikia kwa hivi sasa.
"Mimi nipo na napatikana, sio kama sitaki mazoea bali maisha ambayo ninayoyaishi ni ya kutulia sio kujificha, nikiwa sina vitu vya umuhimu naona bora nitulie nyumbani mara nyingi pia nakuwa na uvivu japo uvivu wangu unanisaidia, hata biashara zangu hazipaswi kuonekana kwenye macho muda wote" ameeleza Matonya
Tazama mahojiano kamili ya Matonya hapa chini kupitia EATV & EA Radio Digital.

