Uwoya afungukia tetesi za kutoka na Kayumba

Alhamisi , 7th Mar , 2019

Mrembo kutoka Bongo Movies, Irene Uwoya amezungumzia juu ya tetesi ya watu mbalimbali kuwa anatoka kimapenzi na mshindi wa Bongo Star Search 2015, Kayumba Juma na kusema hazina ukweli wowote.

Pichani Uwoya akiwa na Kayumba.

Uwoya amesema kuwa mashabiki wake wawe wapole, kama wanataka kumjua shemeji yao watamjua lakini si Kayumba.

Ninachojua ni kwamba watu wengi wako ‘bize’ kujua mimi niko na nani hakuna mtu ambaye watamuacha kumtaja kwenye listi zao kuwa natoka naye kimapenzi hivyo siwashangai na kingine siwezi kutoka na Kayumba mjue hilo", amesema Uwoya.

Uwoya ambaye alifunga ndoa na msanii wa Bongo Fleva, Dogo Janja mwaka uliopita, wawili hao wametengana kutokana na sababu ambazo hawakuziweka wazi ambapo tayari mpaka sasa Dogo Janja amemuweka wazi mpenzi wake mpya.