Alhamisi , 20th Jun , 2019

Mlimbwende kutoka kiwanda cha 'Bongo Movie' Irene Uwoya anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida amesema hatohitaji mchango wowote kutoka kwa mtu yeyote zaidi ya ushirikiano.

Uwoya akiwa na Dogo Janja (kushoto) pamoja na marehemu Ndikumana kulia.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Uwoya kimesema kuwa mwanadada huyo ni kweli ameanzisha kikundi cha 'Whatsapp' na kusema dhamira yake hiyo lakini kutoa kauli ya kusisitiza kwamba hahitaji mchango wowote bali ni ushirikiano tu katika jambo hilo.

"Ni kweli hilo group lipo na amesema kama ulivyosikia hahitaji mchango wowote bali ni ushirikiano tu kutoka kwa wanatasnia, kitu ambacho tumeona sio kibaya ni jambo jema maana ameridhia mwenyewe na sio kwamba tumeshindwa kumchangia", kimesema chanzo hicho. 

Muigizaji Irene Uwoya akifunga ndoa hiyo itakuwa ni ya tatu baada ya ile ya kwanza ambayo alifunga mwaka 2007 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye ni Krish na aliyekuwa raia wa Rwanda na mchezaji wa soka marehemu Hamad Ndikumana na nyingine alifunga na msanii wa muziki wa bongo fleva Dogo Janja ambayo imedumu kwa muda mfupi.