Jumamosi , 15th Feb , 2020

Siku ya jana Februari 14, 2020  "Valentine Day" imeonekana kuwa njema sana kwa Malkia wa uswazi na msanii wa filamu na muziki Snura Mushi, baada ya kurudisha penzi lake kwa Minu Calypto.

Kushoto pichani ni Snura kulia Minu Calypto

Kupitia kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram wawili hao wameonyesha hisia zao baada ya kila mtu kumpost mwenzake, ambapo Snura Mushi ndiyo alianza kufanya hivyo kisha akaandika, "My Valentine nakupenda sana Minhal, ndiyo kwanza nimeanza sasa sijui ninaowakera itakuaje na ahsante sana mpenzi wangu".

Aidha kwa upande wa Minu Calypto naye amepost picha za Snura Mushi halafu akaandika, 

"Nakupenda sana mke wangu Snura kikombe cha plastiki hakivunjiki kwa kudondoka, unajua kiasi gani niliku-miss, hata majembe yalimayo pamoja kuna muda yanagongana mpenzi na kwako nina mapenzi ya mswaki sitaki mwengine achangie".

Wawili hao wameripotiwa hawakuwa na maelewano mazuri tangu mwaka jana walivyoachana, japokuwa sababu za kuachana kwao hazikuwekwa wazi.