Alhamisi , 23rd Jan , 2020

Video Vixen na mwanamitindo Lecandy, amefunguka na kusema anampenda sana msanii Barakah The Prince, hata kama ana mpenzi wake Najma, yupo tayari kuwa hata mke wa pili.

picha ya msanii Barakah The Prince

Akieleza hayo kwenye show ya eNewz ya East Africa TV, ambayo inakuwa hewani kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa 12:00 jioni, Lecandy amesema yeye na Barakah ni zaidi ya washikaji na anajiamini atakuwa wake.

"Kitu kikubwa ambacho nakiamini katika Dunia hii ukimtafuta mwanaume ambaye ni wa peke yako utakuwa ni uongo maana hakuna, sisi waislamu wanawake tutaolewa watatu au wanne kwa mwanume mmoja, nipo tayari kuwa mke wa pili kama kutakuwa na heshima,upendo na mapenzi popote, naweza kuwa nyumba moja na Najma" ameeleza Lecandy.

Kwa upande wa Barakah The Prince baada ya kusikia taarifa hizo amesema kuwa "Kuwa na mwanamke mwingine tofauti na Najma nitamuona ni chizi, kwa sababu sina mpenzi zaidi ya huyo ila huwezi kukataza watu kupenda kwa kuwa mimi ni maarufu japo wengine wana matamanio ya kibinadamu".

Pia amesema mwanamke huyo amefanya naye kazi, katika video ya wimbo wake mpya ambao anatarajia kuuachia siku za hivi karibuni