Wakazi awataka wanasiasa kuacha shobo

Jumatatu , 2nd Dec , 2019

Msanii anayefanya muziki wa HipHop Bongo, Wakazi, amewataka wanasiasa nchini Tanzania, kuacha shobo na sio kila jambo lazima walihusishe na masuala yao ya kisiasa.

Pichani ni msanii wa HipHop Wakazi

Kupitia 'post' aliyoiweka katika mtandao wa Instagram, baada ya kumalizika kwa pambano la Mtanzania Hassan Mwakinyo, dhidi ya raia wa Uphilipino Arnel Tinampay.

"Mambo ya kuweka siasa kwenye michezo, tutakuwa hatuendelei wala kupiga hatua na  mnatukata stimu wengine, acheni shobo" ameandika Wakazi.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Wakazi amesema suala la siasa lisihusishwe na masuala mengine.

"Suala la siasa na shobo nimesema kila wakati wanasiasa huwa wanajihusisha au kuhusika  na mambo hata yasiyokuwa ya siasa na kupenyeza usiasa humo, jambo ambalo linaweza kugawa mashabiki" amesema Wakazi.

Aidha ameendelea kusema  "kwa sababu sio kila mtu anapenda hayo mambo na tukileta siasa kwenye jambo tofauti tutafanya vitu vingine visiendelee, wanasiasa wapunguze shobo sio kila kitu kujipendekeza kwa viongozi wakubwa".