Ijumaa , 27th Mar , 2020

Msanii wa filamu na mfanyabiashara Faiza Ally, amewajibu watu wanaomdiss kwa kusafiri bila kuhofia ugonjwa wa Corona, kwa kusema kama anawaona watu hao watakavyomnanga kama wakisikia amefariki na ugonjwa huo.

Picha ya Faiza Ally

Faiza Ally ambaye kwa sasa yupo nchini Thailand, ameeleza hayo kupitia mtandao wa Instagram, kwa kuwajibu mashabiki waliokuwa wana-comment kwenye picha zake, kuhusu kusafiri nje ya nchi wakati tahadhari zinasema sio lazima kusafiri ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

"Naona comment zenu zote, kama nawaona watu wakisikia Faiza kafa na Corona watasema ndiyo akome bora angetulia, kuja huku kufanya kazi haina maana kama sioni hii Corona na Serikali ya huku watu wanafanya kazi mimi nani nipinge, mnatambua kwamba kuna maisha baada ya Corona, naomba mniache kila mtu anajua hali ya maisha yake" ameandika Faiza Ally.

Aidha ameendelea kueleza  "Nyinyi wenye mishahara kazini, wenye waume au wenye wazazi wenye pesa msijifananishe na sisi ambao lazima tutoke ndiyo tule, zaidi ya sasa nitaanza kublock wote wanaoni-diss niacheni kwa amani" ameongeza.