Msanii Aslay
Kwa kuthibitisha hilo Aslay amepost kipande cha sauti katika mtandao wa Instagram, akiwa anamuuliza mzazi mwenziye kama ni kweli amempiga kisha akaandika.
"Nimesikitishwa sana na vitendo vya kupangwa vyenye nia mbaya dhidi yangu, jioni ya leo wamesambaza video ikidai nimempiga mzazi mwenzangu ni habari ya kizushi mno, sijamgusa kwa namna yoyote ile, ninachokifahamu kuna watu walifika nyumbani kwangu na kuanza kufanya fujo kwa sababu zao" ameandika Aslay.
"Sitaongea mengi najua ukweli utajulikana tu, kinachosikitisha sana kwangu na kwetu kama jamii, ni jinsi vyombo vya habari vinavyoweza kutumika kusambaza uongo, chuki na kuharibu majina ya watu na biashara zao ila Mungu pekee ndiyo shahidi wa ukweli" ameongeza.

