"Wanawake tunajidhalilisha sana" - Isha Mashauzi

Alhamisi , 13th Feb , 2020

Mkali wa miondoko ya Taarabu Isha Mashauzi amefunguka na kusema wanawake wanajidhalilisha sana wanapofikia hatua ya kudanga na kuuza mwili wao ili wapate pesa.

Picha ya msanii wa Taarab Isha Mashauzi

Isha Mashauzi amesema hayo kupitia kipindi cha Mama Mia kilichoruka live leo Februari 13, 2020, maeneo ya Mwananyamala jiji Dar es Salaam.

"Maisha yangu yote sijawahi kudanga hata wigi hili nimevaa kwa hela yangu na hela ya mashabiki, huwa najisikia vibaya nikimkuta mtoto wa kike anauza mwili au anadanga, niwaambie tunajidhalilisha sana, hatuwawekei maisha mazuri watoto wetu" amesema Isha Mashauzi.

Aidha msanii huyo ameongeza kusema  "Mimi ni mwanamke wa kwanza kuimba Taarab, kumiliki bendi, na ndiyo wa kwanza kumiliki gari kwa hela yangu mwenyewe na wala sikwenda Chuo Kikuu bali huwa napita kama njia".