Alhamisi , 18th Apr , 2019

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Q Chillah ameweka wazi kiwango cha elimu cha watoto wake, ambacho mwenyewe amesema si cha kawaida licha ya changamoto nyingi alizopitia, na ndio wanampa nguvu ya kutokata tamaa.

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Q Chilla amesema kuwa wawili miongoni mwa watoto hao wamepata division 1 ya 0, ndio wanaompa nguvu ya kuzidi kupambana.

Akimwambia Big Chawa Q Chillah amesema:

 

“Kwanza nawakumbusha nina watoto, wawili, watatu, wanne, lakini nina wawili ambao wamepiga division one ya one, ya ziro, ambo wamepitia changamoto nyingi sana. Wanataniwa kuwa baba yako alikuwa mvutaji lakini katika changamoto hizo, najaribu kupambana nao, kwa sababu I see an image of, I see God”, amesema Q Chillah.

Q Chillah ambaye kwa sasa bado anakomaa na game ya muziki, amesema kwamba watoto wake hao muda mwingine humwambia ni jinsi gani wanajivunia naye kama baba yao, licha ya kwamba amepitia magumu yenye kukatisha tamaa.