Watu waanza kupora mali za Godzilla

Alhamisi , 21st Feb , 2019

Watu wasiofahamika wamevamia na kuichukua acount ya instagram ya marehemu Godzilla, kitendo ambacho kimewashtua na kuwasikitisha wengi.

Mmoja ya watu waliyeumizwa na kitendo hicho aliamua kumfuata Fid Q na kumtaarifu kuhusiana na kupotea kwa akaunti yake, ndipo Fid Q akaamua kuujulisha umma ambapo amesema haya,
 

Ikumbukwe kwamba hapo jana Februari 20 imetimia wiki moja kamili, tangu Godzilla alipofariki dunia Februari 13 kutokana na kusumbuliwa na tumbo pamoja na presha na kisukari kupanda.