Jumanne , 29th Oct , 2019

Raia kutoka China, anayeishi nchini Juma Sharobaro, ameeleza mipango ya kuwachukua mastaa wa kitanzania kama Wema Sepetu, Idris Sultan, Linah na Lady Jaydee, kuwapeleka China kwa ajili ya kuwa mabalozi wa Lugha ya Kiswahili na kuitangaza Tanzania.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Juma Sharobaro amesema kuwa itakuwa ni njia nzuri kuwachukua mastaa hao na kujadiliana, kuhusu kuwapeleka katika nchi hiyo.

"Nafikiri kwenye 'Platform' yetu tuliwahi kushirikiana na mastaa wengi tofauti kama Wema Sepetu, Linah , Idris Sultan na Lady JayDee kwa hiyo itakuwa njia nzuri kuwapeleka China kujadiliana na kuwasiliana kwa kina kirefu zaidi, lakini kwa sasa mipango bado haijajadiliwa labda siku za mbele" amesema Juma Sharobaro.

Pia Juma Sharobaro amekataa kufananishwa na wajina wake Juma Lokole kwa kusema, huwa anamuona mitandaoni ana anajihusisha na mambo ya udaku na umbea zaidi ila yeye yupo kwenye upande wa muziki japokuwa wanashea jina moja la Juma.