Zilibaki dakika chache kufa - Roma Mkatoliki

Tuesday , 12th Sep , 2017

Rapa Roma Mkatoliki ambaye sasa anafanya vyema na ngoma yake 'Zimbabwe' amefunguka na kusema kuwa ilifika wakati aliamini kuwa zimebakia sekunde kadhaa kuweza kufariki na kuambatana na baba yake mzazi ambaye alifariki Septemba 12, 2002

Roma Mkatoliki amesema hayo leo ikiwa imetiamia miaka 15 toka baba yake mzazi Mzee Mussa alipofariki dunia kipindi ambacho yeye Roma Mkatoliki bado alikuwa mdogo, hivyo ametumia siku hiyo kumuombea apumzike salama na kumpa simulizi juu ya mambo aliyopitia na kudai kuwa katika kipindi chote hajawahi kupitia mambo magumu kama mwaka huu.  

"Kama unanisikia ni miaka 15 sasa imepita, ni imani yetu kuwa upo kwenye makazi mema nasi tunazidi kukuombea uwe sehemu salama huku tukiamini ipo siku tutaungana na wewe tena kama familia, baba uliniacha nikiwa mdogo kiasi, lakini nilikuwa na ndoto kubwa katika maisha yangu mtoto wako nimepitia mambo mengi makubwa hasa mwaka huu ilifika kipindi niliamini zimesalia dakika chache niungane na wewe lakini hayakuwa mapenzi ya Mungu, nikaungana na Mama na tunaendelea na maisha yetu Duniani hapa" aliandika Roma Mkatoliki 

Rapa Roma Mkatoliki mwanzoni mwa mwezi April alitekwa na watu wasiojulikana na kuteswa kiasi cha kuvunjwa mpaka kidole chake cha mwisho na kisha kujakupatikana siku ya tatu akiwa yeye na wenzake huku wakiwa na majereha mbalimbali kwenye miili yao.  
Itazame hapa ngoma yake ya kwanza kutoka baada ya kutekwa ambayo imeweza kujibu maswali kadhaa ambayo watu walikuwa wakijiuliza kipindi alipokuwa ametekwa na yaliyomkuta kwa hao watekaji.