Jumanne , 16th Oct , 2018

Msanii wa muziki wa Bongofleva, Juma Mussa maarufu 'Jux' hatimaye amefunguka kuhusiana na madai ya kutomlipa msanii wa HipHop, Chidbenz baada ya kutumbuiza katika 'show' ya 'In Love & Money' iliyoandaliwa na yeye mwenyewe Jux pamoja na Vanessa Mdee.

Akipiga stori na www.eatv.tv, Jux amesema Chid Benz hakuwa kwenye listi ya wasanii wanaotumbuiza katika tamasha hilo, zaidi alimfuata 'backstage'(nyuma ya jukwaa) wakati 'show' ikiendelea na kumuomba kutumbuiza, hivyo hafahamu madai anayoyatangaza yametokana na makubaliano gani.

Kwanza kabisa Chid hanidai pesa yoyote kwasababu ile 'show' tulivyofika Dar tulikua tayari tumepanga wasanii watakaotumbuiza, hatukuwa na mdhamini, hata wale wasanii baadhi yao kuna vitu tulikua tunawafanyia lakini hatukuwalipa hela, wengi walikuja kutusapoti kama wasanii wenzetu”, amesema Jux.

Chid alinifuata 'backstage' na akasema braza naweza kufanya kitu kwa mashabiki, nikamuheshimu kama braza wangu na msanii mkubwa katika tasnia yetu, akapanda stejini, asubuhi ananipigia ananiambia braza mimi nimefanya 'show' lakini sijapata chochote nikamwambia ok! nitakupa chochote kama asante, ila haikuwa katika maelewano yetu kiasi kwamba anaenda kulalamika kwenye vyombo vya habari kwamba ananidai”, ameongeza.

Kuhusiana na hali ya msanii Chid Benz ilivyo kwasasa, Jux amesema anasikitishwa kumuona msanii huyo akitumiwa katika mambo maovu ambayo hayawezi kumjenga kimaendeleo badala yake imekuwa ni utani unaoendelea kuwafurahisha mashabiki.

Mimi nasikitika kumuona Chid alivyo, naomba tumtumie kumuendeleza na kumjenga, nikipata muda nitamtafuta kama ni pesa nitampatia ila sio kwaajili ya 'show' sikumuita na sikupanga

Msanii Jux anajipanga kuja na album yake mpya kwa mara ya kwanza, itakayoenda kwa jina la 'IN LOVE' anayopanga kuiachia mwakani.