Alhamisi , 26th Dec , 2019

Mwanamke mmoja ambaye ni raia wa China, Teresa Xu,  ameishtaki Hospitali moja nchini humo kwa kukataa kufunga kizazi chake kwa kile alichokieleza kuwa bado hajaolewa pamoja na kujipa nafasi ya kutosha kuendelea na kufanya kazi kupitia taaluma yake.

Sheria

Teresa Xu anatajwa kufika kwenye Hospitalim  hiyo 2018 akiwa na nia ya kugandisha mayai yake katika kipindi ambacho anataka kuweka kipaumbele kwa taaluma yake.

"Nilikuja hapa kwa ajili ya kupata huduma ya kitaalam lakini badala yake nimepata mhudumu anayenisihi niachane na kazi yangu na nipate mtoto" amesema Xu

Jumatatu, Mahakama Beijing ilisikiliza kesi iliyowasilishwa na Bi. Xu dhidi ya Hospitali hiyo.

Kwa mujibu wa Uongozi wa Hospitali hiyo umesema haukufanya hivyo kutokana na sababu za kisheria za nchi hiyo.

Source BBC Swahili