Akamatwa kwa kubaka wanawake 40 ndani ya mji mmoja

Alhamisi , 11th Jun , 2020

Moja kati ya habari ambayo imetawala kwenye vyanzo mbalimbali vya habari nchini Nigeria, inaeleza kukamatwa kwa mwanaume mmoja ambaye anadaiwa kubaka wanawake 40 ndani ya mji mmoja kwa muda wa mwaka 1.

Mikono ikiashiria mtu amekamatwa na kushikiliwa na jeshi la polisi

Mtuhumiwa huyo amefikishwa kituo cha polisi cha mji wa Kano, ambapo mwanamke mmoja mkazi wa Dangora alimkuta amejificha katika chumba cha kulala watoto, kisha akataka kukimbia lakini alimuitia majirani ambao walimsaidia kumkamata na kumfikisha polisi.

Kiongozi wa Afisa Uhusiano wa Umma DSP Abdullahi Haruna amedhibitisha kupatikana kwa mtuhumiwa huyo kwa kusema  "Siku ya Jumanne polisi wamemkamata Muhammad Alfa mwenye miaka 32, wakati wa mahojiano mwanaume huyo alikiri kubaka wanawake zaidi ya 40 kwa mwaka kuanzia wasichana, wanawake walioolewa wazee pamoja na kushambulia watoto walio na umri chini ya miaka 10". 

Aidha Chifu wa mji huo Ahmadu Yau amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni ishara ya maendeleo katika mji wao na watu wamefurahia na wanatumaini haki itatendeka dhidi yao.

Vyanzo : Pulse.ng , All Africa.com , Saharareporters.com , Guardian.ng , Daily Times.ng ,