Amber Rutty ajitokeza na kueleza mazito kwa wabaya

Jumamosi , 6th Jul , 2019

Mmoja wa wasichana aliyejipatia umarufu baada ya kuvuja kwa picha na video za utupu mitandaoni, Amber Rutty ameandika ujumbe mzito, na kuwachana wale wanaondelea kumfanya aonekane mbaya mitandaoni.

Amber Rutty

Amber rutty ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram, baada ya kuendelea kuzagaa kwa video zake za faragha mitandaoni.

"Habari, nasikitishwa sana na baadhi ya vitu vinavyofanywa na watu wanaotumia matumizi mabaya ya mitandaoni ili nionekane mkosefu kila leo. Nakumbuka suala zima lililowahi kutokea mpaka kupelekea mamlaka husika kutuchukulia hatua, tukasota Segerea na mpaka leo kesi ipo mahakamani kuhusu hizo picha na video chafu, tumechanangyikiwa kiakili mpaka kiafya. Ombi letu ni kuomba anayehusika na hili jambo aache mara moja"

Tukio la kuvuja kwa picha hizo mitandaoni zikimuonyesha Amber Rutty na mpenzi wake zilivuja mwezi wa kumi, mwaka jana.

Na siku ya jana ilisambaa tena video nyingine mitandaoni kati ya Amber Rutty na mume wake.