Jumatano , 13th Mar , 2019

Fredrick Ochieng'  kutoka nchini Kenya ana matumaini kuwa siku moja afya yake ya kawaida itarejea licha ya kwamba amepoteza uume wake kwa miaka tisa sasa.

Bwana, Fredrick Ochieng'.

Ochieng' amesema kuwa alikuwa mzima wa afya hadi mwaka wa 2010 alipoanza kuhisi kujikuna katika sehemu nyeti kila mara.

Ochieng' ambaye alifiwa na mkewe miaka kadhaa iliyopita, anasema  amekuwa akipokea matibabu katika hospitali moja kule Muhoroni ila hajawahi kupata nafuu.

"Nilianza kujikuna kwenye sehemu nyeti, kisha nikawa na kidonda kilichochipuka na kusababisha uume wangu kukatika," amesema Ochieng'.

Ochieng' amesema madaktari wameshindwa kubaini anaugua ugonjwa upi ila kwa mara ya kwanza walidhani ulikuwa ugonjwa wa saratani.

Kwa sasa Ochieng' hana uume wake ila anatamani sana aoe tena, apate mke ambaye atampikia, amfulie na atunze watoto wake bila kutaka kushiriki ngono.