Jumatano , 20th Mar , 2019

Mwanamme mmoja wa kijiji cha Mureku eneo la Navakholo kaunti ya Kakamega nchini Kenya anaishi kwa upweke baada ya mkewe kumwacha kwa tetesi kuwa hana sehemu zake za siri.

Alfred Sifuna.

Alfred Sifuna (30) anaishi kwa upweke na uchungu baada ya kuvamiwa na kikundi cha watu alipokuwa barabarani na kumuibia pesa kabla kuzinyofoa sehemu zake za siri na kutoroka nazo huku sababu ya kutendewa unyama huo ukiwa hazijulikani.

"Nilivamiwa nikitoka sokoni na watu ninaowajua, wengine wao ni majirani wangu, walinibeba na kunibana kwa nguvu kisha wakaniibia pesa nilizokuwa nazo kabla yao kunivua nguo na kukata sehemu yangu ya siri ambayo walitoroka nayo sijui kile walichoenda kufanyia." amesema sifuna.

Ameongeza kuwa, "Niliachwa na mke ambaye amehamia sehemu nyingine baada ya kugundua sina sehemu zangu za siri, kwa hivyo siwezi kumtosheleza ipasavyo, nashinda nikitembea na leso kama mtu ambaye ametahiri na sasa naomba serikali pamoja na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kuingilia kati na kunisaidia kupata haki".

Sifuna anadai kuwa licha ya kuripoti kesi hiyo katika kituo cha polisi cha Navakholo, hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya wahuni hao kwani walikamatwa na kuachiliwa kwa dhamana jambo ambalo limepelekea yeye kutishiwa maisha na watu hao.