Atiwa mbaroni kwa kukata uume wa mwenzake

Alhamisi , 18th Jul , 2019

Mkazi mmoja wa jiji la Florida nchini Marekani aitwae Alex Bonella, mwenye miaka 49, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumkata Uume mwanaume mwenzake.

Kwenye picha ndogo ndiye mtuhumiwa

Mtuhumiwa huyo alifanya tukio hilo siku ya Jumapili, na alikata Uume wa mwanaume mwenzake kwa kutumia mkasi kwa sababu alikuwa anaamini mwanaume huyo alilala na mkewe.

Ofisa wa polisi katika kituo cha Gilchrist County Sheriff, wamesema taarifa hizo walizipata kutoka kwa jirani wa mtuhumiwa huyo, ambaye aliripoti polisi kuhusu mtuhumiwa huyo kumuomba mkasi na kumshikia silaha.

Aidha muathirika wa tukio ambaye yupo hospitali kwa sasa amesema Alex Bonilla alienda nyumbani kwake na kumtishia kumuua huku amemshikia bunduki kama akikataa kufanya atakavyo, na kumlazimisha kulala chini na kumtolea mkasi na kisha kumkata Uume wake.

Hata hivyo mtuhumiwa mwenyewe wa tukio hilo Alex Bonilla amesema mwanaume huyo alifanya mapenzi na mke wake nyumbani kwake mwezi wa tano mwaka huu, na mpaka sasa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa mawili, moja ni kufanya uhalifu wa kikatili, pili ni kushambulia kwa kutumia silaha.