Auza nyeti zake baada ya kukosa udiwani

Jumatatu , 11th Feb , 2019

Mwanamume mmoja aliyebwagwa kwenye kinyang’anyiro cha udiwani katika kaunti ya migori anayedai kuwa amefilisika, ametangaza kutaka kuuza nyeti zake kwa Ksh 500,000 ambazo ni sawa na zaidi ya milioni 11 za Tanzania.

Mwanaume huyo anayejulikana kwa jina la Ian- Harriet Kowiti kutoka eneo la Uriri, Kaunti ya Migori amesema kuwa amechoshwa na maisha ya ukata, na sasa ameamua kutafuta pesa kwa kuuza korodani moja.

Pia mwanaume huyo amesema kwamba yuko tayari kuuza figo moja kwa Sh1.5 milioni za Kenya ambazo ni sawa na zaidi ya milioni 34 za Tanzania, kwa mteja wa nchini humo, au mara tatu ya pesa hizo kwa mteja kutoka nje ya nchi.

“Ina haja gani kuwa na korodani mbili kati ya miguu yangu wakati hata nikiwa na moja bado naweza kufanya ‘kazi’ vyema? Nataka kuuza kwa kuwa nimekosa pesa na pia sihitaji korodani mbili ili kuishi. Najua kuna mtu mahali amekosa mtoto kwa ajili ya tatizo kama hili,” amesema Kohiti.

Katika uchaguzi uliopita, Kowiti ambaye ana miaka 27 alijaribu kuwania kama mgombea huru katika wadi moja, lakini akabwagwa, amesema kuwa anapanga kuuza sehemu hiyo ili kuboresha maisha yake.