Azika mgomba wa ndizi ili aoe mke mwingine

Jumanne , 12th Mar , 2019

Familia moja kutoka kijiji cha Lubai, Kaunti ya Kakamega nchini Kenya imelazimisha kijana wao wa kiume kuzika mgomba wa ndizi ili kuashiria mwili wa mke wake ambaye alitoweka miaka 13 iliyopita.

Picha ya mgomba.

Bernard Munase alishawishiwa na wazee wa jamii ya Waisukha kufanya sherehe za kumzika mkewe kulingana na tamaduni za jamii hiyo ili aweze kuoa mke mwingine.

Wazee wa jamii hiyo wamesema walihitajika kufanya sherehe ili kumpa fursa kijana wao kuoa mke mwingine. Munase amesema amemtafuta mkewe kila pembe bila mafanikio na sasa hana imani tena iwapo atampata akiwa hai.

"Mungu alikuwa ametubariki na mtoto wa kiume kabla mke wangu kujatoweka, mimi pamoja na jamaa zangu tumemtafuta kila mahali bila mafanikio", amesema Munase.

Baada ya sherehe hiyo, wazee hao wa jadi wamesema Munase sasa yuko huru kuoa mke mwingine huku wakiamini yule wa awali aliaga dunia.

Bofya link hapo chini kutazama video.