Dereva aliyemuachia Nyani kuendesha Basi afukuzwa

Jumatatu , 8th Oct , 2018

Dereva aliyemruhusu Nyani kuendesha basi lililokuwa limebeba abiria nchini India hatimaye amefukuzwa kazi baada ya video ya tukio hilo kusambaa mitandao ya kijamii na kuwafikikia serikali na wamiliki wa basi hilo.

Picha ya dereva na Nyani

Katika video iliyokuwa ikisambaa mitandao ya kijamii ilimuonesha dereva Bw. Prakash mwenye umri wa miaka 36, akimuachia nyani kuketi juu ya uskani wa basi hilo na kuendesha huku dereva huyo akionekana kufurahishwa na kitendo hiko.

Msemaji wa kampuni ya usafiri wa barabara nchini India Bw. Kartanaka amesema kitendo hicho kimesababisha wamiliki na serikali kumfukuzwa kazi dereva wa basi hilo ambalo lilikuwa na abiria takribani 30, kitendo ambacho kina kinzana na kanuni na taratibu za usafiri nchini humo.

Wasomaji wa mitandao ya kijamii kutoka nchini humo wameoneshwa kukasirishwa na kitendo cha kukamatwa kwa dereva huyo, huku wengi wao wakidai alipaswa kuonywa na sio kufukuzwa kazi.

"Angepewa onyo na aambiwe asirudie, mmoja wa wasomaji aliandika katika ukurasa wake wa Twitter".

Kwa mujibu ya walioshuhudia, wanasema nyani alipanda gari na abiria mwingine lakini akakataa kukaa nyuma na akachagua kiti cha dereva,nadaiwa kwamba nyani huyo alipofika kwenye kituo chake alishuka na kumuacha dereva akiendelea na safari yake.