EATV kutambulisha kipindi kipya

Jumatatu , 15th Jul , 2019

Kituo cha East Africa Television pamoja na kampuni ya uzalishaji wa maudhui ya sauti na video ya Kwetu Studio, zinatarajia kutambulisha kipindi kikubwa cha masuala ya vijana nchini kitakachojulikana kama 'KIJANA ONGEA'.

Kipindi kipya cha KIJANA ONGEA

Kipindi hicho kinatarajia kuruka kuanzia Jumapili ya wiki hii, Julai 21, saa 1:00 usiku na marudio ni kila Jumatatu, saa 9:30 alasiri na Alhamisi, saa 6:30 mchana.

Vijana watakaohusika katika kipindi hicho ni kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Mtwara, ambao wataenda sambamba na kujadili mada mbalimbali ikiwemo elimu ya ufundi, biashara ndogondogo, habari za vijana waliofanikiwa kutoka vyuo mbalimbali vya ufundi (VETA) pamoja na vituo vya mafunzo ya ujasiriamali.

Usikose kutazama kipindi hiki kipya ili ujifunze ujuzi mbalimbali katika maisha.