Emmett Till alivyodhulumiwa uhai wake

Alhamisi , 18th Oct , 2018

Tahadhari, picha ya kuogopesha chini.

Emmett Louis Till alizaliwa Julai 25, 1941 huko Chicago nchini Marekani, akiwa mtoto wa mwanajeshi Louis Till aliyezaa na Mamie Elizabeth Till-Mobley.

Mtoto Emmett Till

Mnamo mwezi Augosti 1955, Emmett Till akiwa na umri wa miaka 14, alikwenda kutembelea ndugu zake huko Mississippi, siku moja alikwenda katika duka ambalo lilikuwa likimilikiwa na raia wa kizungu alyejulikana kwa jina la Bryant. Alipokwenda dukani alikutana na mke wa Bryant, Nicole, ambaye alikuwa akiuza duka hilo, kilichoendelea hakikujulikana lakini mwanamke huyo alimtuhumu kumdhalilisha kingono ikiwemo kumshika matiti.

Baada ya siku kupita mume wa Nicole, Roy Bryant na kaka yake J.W Millam, walimchukua Emmett kutoka nyumbani kwao, huku ndugu yake mmoja akishuhudia, walimchukua na kwenda naye mahali ambako walimpiga vibaya na kisha kumpiga risasi kichwani, wakamzungushia waya shingoni kisha wakamtupa kwenye mto  Tallahatchie.

Baada ya siku kupita mwili wa Emmet ulipatikana ukiwa umeharibiwa vibaya, ukarudishwa Chicago kwa mama yake ili kuendela na shughuli za mazishi, mama yake aliacha mwili wa mtoto wake ili watu waone jinsi alivyouawa kikatili na watu weupe.

Msiba wa Emmett ulihudhuriwa na watu wengi ikiwemo wanaharakati wa kutetea haki za watu weusi, ambao walikuwa wakinyanyaswa sana miaka ya nyuma huko nchini Marekani.

Baada ya hapo ilifunguliwa kesi dhidi ya waliohusika na tukio la kumuua Emmett, Roy Bryant na kaka yake J.W Millam, lakini watuhumiwa hao waliachwa huru.

Miaka ya hivi karibuni mwanamke aliyemtuhumu Emmet kuwa alimdhalilisha kwa kumshika matiti, Bi. Caroline Bryant, alinukuliwa akisema kwamba mtoto huyo hakuwahi kumfanyia hivyo kama alivyotoa ushahidi hapo awali, isipokuwa alidanganya tu na kushinikizwa.

Kifo cha Emmett kiliibua hisia kali kwa wanaharakati wa kutetea haki za watu weusi, hasa baada ya kushuhudia mwili wa Emmett jinsi ulivyojeruhiwa vibaya, na kubaki kama icon ya harakati za watu weusi nchini Marekani.                          

                             ​​​​​​

                                            Mwili wa Emmett ulivyojeruhiwa na wauaji wake

                 Mama yake Emmett akiaga mwili wa Emmet huku sanduku lake likiwa limeachwa wazi

       

               

                              Bi. Caroline Bryant ambaye alimtuhumu Emmett kumdhalilisha kingono

                                  

                                 Wazungu waliotuhumiwa kumuua Emmett, Roy Bryant na kaka yake J.W Millam