Fahamu kuhusu video za faragha zitumwazo mtandaoni

Alhamisi , 25th Apr , 2019

Kutokana na ukuaji wa kasi wa teknolojia hivi sasa, kila kitu ninaweza kufanyika pasipo hata watu kuonana kwa macho.

Baadhi ya mitandao ya kijamii

Hiyo pia hutokea hata kwa wapenzi ambao wanaweza kuwasiliana moja kwa moja bila kuonana, ikiwa ni pamoja na kutumiana picha, sauti na video kwa lengo la kufurahishana. Mara nyingine picha hizo zinaweza kuwa si nzuri sana kutumwa mtandaoni kwa kuwa ni za faragha.

Akilielezea hilo katika kipindi cha Mjadala cha EATV, mtaalam wa masuala ya kimtandao, Maxence Melo amesema kuwa kitu kinachosababisha ujumbe wowote kuvuja mtandandaoni pasipo wahusika kusambaza ni kuingiliwa kwa mawasiliano ya kimtandao.

"Si rahisi kwa ujumbe wowote wa faragha kuvuja mtandaoni pasipo watu waliotumiana kuhusika au kuwepo kwa pengo linaloruhusu kwa sababu unapokuwa unatuma ujumbe wowote mtandaoni, unaweza ukaingiliwa na mtu wa kati ambao ni wadukuzi", amesema.

"Lakini pili, kifaa cha mhusika kinaweza kikawa ni sababu pia ya kuvuja kwa sababu watu wengi wanaotumia hasa simu za android wanapakua 'application' mbalimbali ambazo zingine zinachukua taarifa za mtumiaji na kutuma kwa watu wengine bila ya mtumiaji kujua", ameongeza.

Mtaalam huyo amesisitiza kuwa si salama kwa wapenzi kutumiana picha mtandaoni hata kama wanaaminiana na kusisitiza kuwa ni kosa kwa mujibu wa sheria za mtandao, kipengele cha 14 kwa mtu kuchukua video ya faragha na kuitengeneza kwa lengo lolote na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 7 au faini isiyopungua milioni 20.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.