Faida za kushirikisha wazazi kutafuta mchumba

Alhamisi , 20th Jun , 2019

Tumezoea katika miaka ya hivi sasa kuona vijana wanajitafutia wenyewe wapenzi wao na kisha kuwatambulisha kwa wazazi baada ya kukubaliana.

Mahusiano

Lakini miaka kadhaa iliyopita hakukuwepo na mambo kama hayo kutokana na kukomaa kwa mila na desturi za makabila.

Katika kipindi cha DADAZ cha EATV, imezungumzwa mada iliyohusu umuhimu wa kuwashirikisha wazazi katika namna ya kutafuta wachumba na kufunga ndoa, ambapo mageni, 'Pasto' Naomi Mhamba ambaye ni mzazi na mshauri wa mahusiano amezungumzia kwa kina katika kipengele cha 'Mtu kati'.

Pastor Naomi amesema kuwa ni muhimu wazazi kushirikishwa kwakuwa wamepewa dhamana na Mungu katika kuwalea watoto hadi wanakua. Sababu nyingine ambayo mzazi wanapaswa kushirikishwa ni kutokana na kwamba wanawafahamu watoto wao vizuri kuliko mtu mwingine yoyote.

Mtazame hapa chini akizungumzia sababu zingine ambazo zinaelezea umuhimu wa wazazi kushirikishwa katika mahusiano ya watoto wao.