Jinsi ya kuishi na mpenzi uliyempenda kimuonekano

Ijumaa , 26th Apr , 2019

Kuna namna nyingi ambazo wapenzi hukutana katika kizazi cha hivi sasa tofauti na kizazi cha miaka ya nyuma. 

Picha ya wapenzi

Kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia na utandawazi, hivi sasa wapenzi hukutana katika mitandao na hata katika mazingira mengine ya nje kama sehemu za starehe na za usafiri.

Katika kulizungumzia hilo, Mtaalam wa Masuala ya Mahusiano, Aunt Sadaka, katika kipindi cha Dadaz cha EATV ameeleza kuwa kinachopelekea mtu kumpenda mwenzie pasipo kuvutiwa naye ni matamanio ya nafsi.

"Wengi huwa tunapata mhemko tunapomuona mtu na moyo unadunda, tunadhani yale ndiyo mapenzi, yale huwa ni matamanio tuu. Tunaangukia katika mtazamo wa nje, kwa kuona jinsi mtu anavyoongea lakini kiukweli tunachonkwenda kuishi nacho sio ule muonekano, bali unakwenda kuishi na tabia ya mtu", amesema Aunt Sadaka.

Mtazame hapa akizungumzia zaidi suala hilo.