Kifo chawakaribia kwa kuiba matairi

Jumatano , 13th Mar , 2019

Vijana wawili wamenusurika kifo baada ya kupewa kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira, walipokutwa wakiiba kwenye Yard ya magari.

Akizungumza na East Africa Radio, Mlinzi wa Yard hiyo Ezla Sanga maarufu kama Eze, amesema vijana hao waliingia saa 11 Alfajiri na kuanza kushusha matairi, na ndipo alipoamua kuomba msaada kwa watu waweze kukabiliana nao.

Naye dada wa vijana hao amesema kwamba ndugu zake walikuwa wanajishughulisha na kuuza mipira inayotengenezwa kutokana na matairi ya magari wanayonunua kwa watu mbali mbali.

Vijana hao ambao wamejeruhiwa baadhi ya maeneo, wamepelekwa kituo cha polisi Kinondoni ili kufunguliwa mashtaka.

 

Sikiliza hapa mlinzi na dada wa mwizi wakisimulia