Alhamisi , 19th Sep , 2019

Binadamu tuko na tabia tofauti tofauti lakini utaratibu ndio unasaidia kutuongoza ili tuishi vizuri, ndio maana tunasoma na kujifunza.

Mahusiano

Hivyo hivyo katika mahusiano, kuna vitu vya muhimu vya kuzingatia ili kuyaishi mahusiano yenye upendo, furaha na maelewano. Mshauri wa masuala ya mahusiano, Isack Chalo amezungumzia juu ya umuhimu wa lugha hizo tano kupitia kipindi cha Dadaz cha EATV.

Chalo amesema lugha hizo hutumika kwenye mahusiano ya kudumu, ya muda mrefu na yenye kuleta matokeo kwa wahusika na kwamba zinaweza kutumika hata kwenye mahusiano tofauti na mapenzi.

"Lugha ya kwanza ambayo imeongelewa na wataalam wa mapenzi ni ile kutambua na kumpongeza mtu anapofanya vizuri, hii ni kumpongeza mtu anapofanya vizuri, anapopendeza, kwa sababu kila mtu ana mazuri na madhaifu yake lakini ni vizuri akisifiwa", amesema.

"Lugha ya pili ni suala la kuwa na muda wa kutosha miongoni mwa wahusika katika mahusiano, mahusiano yanadumishwa kutokana na kuwa na muda wa kutosha kujadiliana kuhusu mipango yenu. Lugha ya tatu inayohitajika ni katika mahusiano ni kutoa zawadi, kwa maana ya kwamba wewe unampa zawadi mpenzi wako na yeye anakupa zawadi", ameongeza.

Mtaalam huyo ameongeza kuwa lugha ya nne ni kuhudumiana na kusaidiana, huku lugha ya tano akiitaja kuwa ni habari za mguso, akimaanisha kuwa wapenzi kugusana kunakoonesha kuwa ni watu wa karibu.

Kupata ufafanuzi mzuri wa lugha hizo tano, fuatilia katika video hapa chini.