Jumanne , 25th Feb , 2020

Mshauri wa masuala ya ndoa Mama Terry, ametoa onyo kwa wanawake ambao wanaolewa na wanaume waliowazidi umri kwa kusema watakutana na changamoto nyingi sana kwenye ndoa hiyo.

Picha ya Mama Terry

Akipiga stori na Big Chawa kwenye show ya Planet Bongo, inayoruka kila siku za Jumatatu-Ijumaa kupitia East Africa Radio, kuanzia 7:00 mchana hadi 10:00 jioni, Mama Terry ameshangaa kuona watu wanavyopata tabu pale mwanaume mdogo anapomuoa mwanamke ambaye amemzidi umri.

"Sasa hivi hata watu wazima wanaitwa baby, halafu nashangaa kijana anapooa mtu mzima inakua stori, ila mzee kuoa binti mdogo ni jambo la kawaida, kama unataka kufaidi ndoa lazima muwe watu wenye levo sawa, ambapo mtaweza kucheka na kutaniana, wakina mama wazee kuolewa na vijana kama wa miaka 24 watapata shida kwa sababu yeye kashamaliza mambo mengi ila kijana ndiyo kwanza anakuwa" ameeleza Mama Terry.

Aidha Mama Terry amewazungumzia wale wenye tabia za kupost na kuvujisha picha au video zisizo na maadili mitandaoni kwa kusema, "Nawashangaa  vijana wanaopost picha za utupu au ngono mitandaoni, kwanza kila mtu anao utupu wake labda wajee na kitu kipya, kama ana sehemu za siri tatu ndiyo tutashangaa".