Jumatano , 11th Mar , 2020

Mfalme wa BongoFleva Alikiba amefunguka na kusema, hakuna kitu kinachomuuma kama kufungwa mara mbili mfululizo na Team Mbwana Samatta, katika pambano lao la SamaKiba Foundation, ambalo huwa linafanyika mara moja kwa mwaka.

Kushoto ni Alikiba, kulia Mbwana Samatta

Akizungumza hayo leo Machi 11, 2020, mbele ya waandishi wa habari, wakati anazindua jezi mpya zitakazotumika katika mchezo ujao kati ya Team Kiba na Team Samatta, ambao utachezwa Juni 6, 2020.

"Nina imani safari hii itakuwa tofauti na watu wanatamani kuona wachezaji tofauti kutoka Mataifa mbalimbali na timu kubwa duniani, mara nyingi mchezo huu ulikuwa unatukutia ndani ya mwezi wa Ramadhan, halafu sisi Waislam tunafunga lakini Samatta yeye hafungagi kwahiyo anakuwa ana nguvu sana, pia inaniuma kufungwa mara mbili mfululizo" ameeleza Alikiba.

Mengine zaidi aliyoyaeleza tazama kwenye video hapo chini.