Jumatatu , 16th Mar , 2020

Mchekeshaji na mshehereshaji MC Pilipili, amesema hajawahi kutumia kilevi chochote na hataki kusikia hayo mambo kwa sababu sasa hivi anataka kuwa mtumishi wa Mungu.

Mchekeshaji MC Pilipili

MC Pilipili ameiambia EATV & EA Radio Digital kuwa, haendi kwenye kazi ya Uchungaji kwa ajili ya kufuata pesa bali kwa mlengo wa kumtumikia Mungu.

"Mimi ni Mchungaji mtarajiwa ninajiheshimu na nina nidhamu, kitu kama ulevi kwangu hakipo japokuwa watu wanaona na wanasema ila hawana uhakika nacho, ninaenda kuwa mtumishi wa Mungu na nina misingi hiyo" amesema MC Pilipili.

Aidha akieleza sababu za kupelekea kuwa Mchungaji MC Pilipili amesema "Sasa hivi nimekuwa na uhusiano wa ukaribu zaidi na Mungu, itakuwa kitu kizuri kuwasaidia watu wengine kuweza kujitambua kwenye umuhimu wa maisha yao, na hakuna mwanadamu anayeweza kuleta kitu kipya"