Ijumaa , 6th Dec , 2019

Tory Ojeda mwenye umri miaka 20, ni mwanamke ambaye anaishi jijini Florida, nchini Marekani, ameweka wazi kuwa yupo katika mahusiano, yanayohusisha kuwa na mwanaume zaidi ya mmoja 'Polyamorous'.

Tory akiwa na wanaume zake wote wanne.

Mwanamke huyo ambaye kwa sasa ana ujauzito wa miezi 7, anaonekana kufurahia kuwa na jumla ya wanaume wanne, ambao ni Marc 18, Travis 23, Ethan na Christopher wenye miaka 22.

Tory                                                              akicheza karata na waume zake.

Kupitia chanzo cha habari cha Daily Maily, inadaiwa mwanamke huyo anaishi na wanaume zake wote kwenye nyumba moja, wanafanya shughuli za kijamii pamoja na hata wakitaka kupanga mitoko yao hutoka pamoja.

"Christopher ndiyo Baba halisi wa huyu Mtoto, mara ya mwisho tulivyotoka kimapenzi mapumziko nilikuwa naye, ila yote kwa yote tutamlea pamoja na kila mtu atakuwa Baba" amesema Tory Ojeda.

Aidha Tory ameongeza kuwa "Wote tumefurahia sana na tuna shauku juu ya kumlea mtoto wetu pamoja, sasa hivi tutakuwa watano kwenye nyumba na tunatakiwa kupata mtoto zaidi ya mmoja, tutamlea kama familia moja" ameongeza.

                                                Tory akiwa na Baba halisi wa mwanaye.

Tory Ojeda na wanaume zake wote wanne, wanatarajia kupata Mtoto wa Kike miezi miwili ijayo.