Mpenzi wa Dulla achukizwa alivyojifanya mwanamke

Jumanne , 11th Feb , 2020

Fia Makabila ambaye ni 'EX' wa Dulla Makabila, amesema hajapendezwa na kitendo alichokifanya msanii huyo kwa kujipaka urembo na kuonekana kama mwanamke kisha kupost picha na video mitandaoni.

Picha ya Dulla Makabila katika muonekano wa kike

Fia Makabila amesema anamjua Dulla vizuri, ile sio akili yake bali ameshauriwa na viongozi wake au kampani ya marafiki ambao wanamzunguka, na angefanya tukio hilo wakati wapo kwenye mahusiano asingeweza kumvumilia.

"Yule ni yeye kweli na mimi kama mzazi sijapenda alivyofanya, nafikiri hata mama yake atakuwa hajalifurahia hilo suala, kama akiliona kama mzazi wake, ingenitokea mimi nisingelichukulia dogo na hakuna aliyelifurahia kwa sababu yeye ni mwanaume na vitu kama vile anatakiwa afanye mtoto wa kike" ameeleza.

Aidha Fia Makabila ameendelea kusema  "Dulla Makabila ajitahidi huenda akafika mbali akitumia masuala hayo, anaweza akawa amekaa na viongozi wake au watu wengi watakuwa  wamemshauri afanye hivyo, yeye asingeweza kufanya hivyo akili yake naijua ila angekuwa demu angekuwa mzuri sana".

Pia amesema yeye na Dulla Makabila wameachana mwezi mmoja uliopita, na amekataa kama alikuwa 'Kiben ten' chake kwa kumlea ila walikuwa wanaleana.