Mwanafunzi auawa kwa kushambuliwa na majambazi

Ijumaa , 8th Mar , 2019

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Jomo Kenyatta ameshambuliwa na genge la majambazi na kuuawa alipokuwa akimsindikiza mpenzi wake kuelekea nyumbani.

Picha haihusiani na tukio

Kevin Shawn Mugenda na mpenzi wake walivamiwa wakiwa katika eneo la Highpoint katika barabara kuu ya Thika nchini Kenya Jumatatu Machi 4, 2019.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na moja ya kituo cha habari nchini humo, Mugenda aliuawa baada ya kukataa kuwapatia majambazi hao pesa alizokuwa nazo na simu yake.

Tukio hili linatokea ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya mwanafunzi mwingine kutoka katika chuo hicho kuuawa na genge la majambazi eneo la Gachororo katika mtaa wa Juja, hali iliyopelekea wanafunzi kuulaumu uongozi wa chuo kutowaimarishia ulinzi.